• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Raga ya Uganda yakosa kupanda jedwali licha ya ushindi mkubwa

    (GMT+08:00) 2017-07-18 10:48:09

    Wachezaji wa Rugby Cranes kutoka Uganda walisherehekea ushindi wao mkubwa dhidi ya wenzao kutoka Tunisia wikendi hii katika Legends Rugby Club Turf kufuatia rekodi 78-17 kwenye mashindano ya Afrika Cup Gold.

    Hata hivyo timu hiyo bado haijasonga nafasi kwenye jedwali. Kufikia sasa Uganda imejizolea alama 11, lakini bado imejipata katika nafasi ya tatu jedwalini, mahali ambapo walikuwa mwishoni mwa wiki.

    Kenya, ambao walishinda Senegal 45-25 huko Nairobi, ni ya pili na alama 13 nyuma ya viongozi Namibia ambao wana alama 15. Zimbabwe ni ya nne na alama saba mbele ya Senegal yenye alama 1 na Tunisia inayovuta mkia bila alama yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako