• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitarajia jumuiya ya kimataifa itaongeza nguvu kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-07-18 18:29:09

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, China inatarajia jumuiya ya kimataifa itatoa mchango wa kiujenzi na kuongeza nguvu katika kutatua suala la nyuklia katika peninsula ya Korea badala ya kuweka vizuizi.

    Lu Kang amesema, maendeleo mazuri yaliyopatikana kwenye suala la nyuklia la peninsula ya Korea yalipatikana kupitia mazungumzo, na kwamba uzoefu umethibitisha kuwa upinzani na shinikizo vitasababisha kuongeza hali ya wasiwasi katika peninsula hiyo.

    Jana, Korea Kusini ilitoa mapendekezo kadhaa kwa Korea Kaskazini, ikiwemo kufanya mazungumzo ya kijeshi. Lakini Marekani, Uingereza na Japan nazo zimesema huu si wakati wa kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini, bali zinatakiwa kuongeza nguvu kuishinikiza Korea Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako