• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 5 wa mawaziri wa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia wa nchi za BRICS wafanyika mjini Hangzhou

    (GMT+08:00) 2017-07-18 19:42:45

    Mkutano wa 5 wa mawaziri wa uvumbuzi wa sayansi na teknolojia wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini zinazounda kundi la BRICS umefanyika mjini Hangzhou.

    Mkutano huo wenye kauli mbiu ya "kuongoza uvumbuzi, kuimarisha ushirikiano" umefikia makubaliano mengi muhimu ikiwemo mawasiliano ya sera za uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kufadhili kwa pamoja miradi ya utafiti.

    Kwa mujibu wa mpango wa ushirikiano kati ya nchi za BRICS uliopitishwa kwenye mkutano huo, nchi hizo zitaimarisha ushirikiano kwenye uvumbuzi, kuhimiza ushirikiano kati ya maeneo ya sayansi na teknolojia, kuhamisha na kutumia teknolojia, kuunga mkono uwekezaji katika uvumbuzi, na kufanya ushirikiano kwenye miradi mikubwa ya sayansi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako