• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Magufuli kuzindua miradi 9 ya maendeleo

    (GMT+08:00) 2017-07-18 20:05:01

    Rais John Magufuli anatarajiwa kuzindua miradi tisa ya barabara na uwanja wa ndege ambayo itaunganisha mikoa ya Ukanda wa Kati na Magharibi nchini Tanzania na nchi jirani kwa barabara za lami katika kuchochea harakati za maendeleo ya uchumi wa viwanda.

    Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Ujenzi, Joseph Nyamhanga uzinduzi wa miradi hiyo utafanyika katika mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Singida kuanzia wiki hii.

    Nyamhanga alisema ufunguzi wa barabara ya Kigoma – Biharamulo – Lusahunga yenye urefu wa kilometa 154 utafanyika Biharamulo Mjini mkoani Kagera .

    Aidha, Katibu Mkuu alieleza kuwa ufunguzi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora utafanyika Julai 24 na ufunguzi wa mradi wa Manyoni – Itigi – Chanya wenye urefu wa kilometa 89.3 utafanyika Itigi mkoani Singida Julai 25, mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako