• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Vijana wa Afrika kuanza leo nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-07-19 09:32:00

    Mkutano wa kilele kuhusu Vijana wa Afrika (YouthConnekt Africa) unaoanza leo mjini Kigali, Rwanda na kumalizika tarehe 21, utaangazia masuala ya kuongeza nafasi za ajira kupitia ujasiriamali na kuendeleza ujuzi miongoni mwa vijana.

    Mkutano huo wenye kauli mbiu ya "Kutambua Uwezo wa Vijana wa Afrika" unaojumuisha takriban washiriki 2,500 wakiwemo vijana wajasiriamali 100, umeandaliwa na serikali ya Rwanda, Shirika la maendeleo na biashara la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) na Shirika la Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).

    Waziri wa vijana na teknolojia ya habari wa Rwanda Bw Jean Philbert Nsengimana amesema mkutano huo utahamasisha na kuunga mkono vijana wa Afrika kukabiliana na ukosefu wa ajira kupitia ujasiriamali. Mfanyabiashara mkubwa na mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba ya China, Bw Jack Ma ni miongoni mwa wageni watakaohutubia mkutano huo, pamoja na Rais Paul Kagame.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako