• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa waadhimisha siku ya kimataifa ya Nelson Mandela

  (GMT+08:00) 2017-07-19 09:57:34

  Baraza kuu la 71 la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya Nelson Mandela, kwa kuzingatia kuchukua hatua za kukomesha umaskini.

  Kwenye mkutano huo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, njia bora ya kutoa heshima kwa hayati Nelson Mandela sio maneno wala hafla, bali ni hatua halisi za kuleta mabadiliko duniani.

  Umoja wa Mataifa na Mfuko wa Nelson Mandela wametoa wito kwa watu kote duniani kutoa mchango katika jamii, ili kuleta mabadiliko ya kudumu.

  Mwenyekiti wa baraza la umoja wa mataifa Bw Peter Thomsen ametoa hotuba ikisema, dunia inakabiliwa na matumizi ya mabavu, kuongezeka kwa hali ya kukosekana kwa usawa, umaskini, na mabadiliko ya hali ya hewa, hivyo inahitaji kuenzi moyo wa Nelson Mandela, yaani huruma, moyo mwema na kuheshimu utu wa pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako