• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenzake wa Palestina hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2017-07-19 10:13:17

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Palestina Mahmoud Abbas ambaye yuko ziarani nchini China.

    Rais Xi amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na Palestina, na kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali. Amesema China inaishukuru Palestina kwa kushikilia sera ya kuwepo kwa China Moja, na itaendelea kuunga mkono juhudi za watu wa Palestina za kurejesha mamlaka na haki halali za taifa.

    Rais Xi pia amesema China inapenda kushirikiana na Palestina kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na itaunga mkono makampuni yenye nguvu ya China kuwekeza nchini Palestina, ili kutimiza ushirikiano wa kunufaishana.

    Kwa upande wake rais Abbas amesema, urafiki wa jadi kati ya Palestina na China utadumu, na Palestina inaishukuru China kwa uungaji mkono wake. Amesisitiza kuwa Palestina itaendelea kufuata sera ya China Moja na kuiunga mkono China katika kutimiza umoja wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako