• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yamezea mate umwenyeji wa matukio ya michezo zaidi ya dunia

    (GMT+08:00) 2017-07-19 14:10:30

    Baada ya mafanikio makubwa katika mashindano ya dunia ya chipukizi wasiozidi miaka 18 mjini Nairobi, Kenya sasa imeanza kampeini ya kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya kimataifa zaidi.

    Waziri wa michezo wa Kenya Hassan Wario alisema mafanikio ya toleo la mwisho la mashindano ya chipukizi yaliyokamilika wikendi hii yalidhihirisha uwezo wa Kenya kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa.

    Aidha, Wario anasema mafanikio hayo yaliwanyamazisha wale ambao walidhani Kenya haitafaulu kuandaa mashindano hayo. Waziri huyo anasema utaalamu na uzoefu uliokusanywa kutoka uwenyeji huyo utatumika wakati Kenya itaandaa mashindano ya Mataifa Bingwa Afrika (CHAN), mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako