• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Conte atia mkataba mpya Chelsea

    (GMT+08:00) 2017-07-19 14:11:25

    Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuwanoa mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu ya England.

    Conte katika msimu wake wa kwanza ameisadia Chelsea kutwaa ubingwa wa England kwa kushinda michezo 30, na kucheza fainali ya michuano ya kombe la FA licha ya kufungwa na Arsenal katika fainali.

    Baada ya kusaini mkataba huo mpya Conte alielezea furaha yake akisema wajibu wake mkubwa ni kuhakikisha klabu hiyo inabakia miongoni mwa vilabu bora zaidi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako