• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara China wapigwa msasa

    (GMT+08:00) 2017-07-19 19:06:46

    MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza mkakati wa kuwapiga msasa wafanyabiashara kutoka China ili watambue kodi wanazotakiwa kulipa serikalini na taratibu wanazotakiwa kufuata wakati wanapokuwa wanaishi nchini.

    Kwa kuanzia jana, TRA ilianza kuwaelimisha wafanyabiashara wa China, wanaofanya kazi katika wilaya ya Ilala.

    Meneja wa Elimu kwa Walipa Kodi wa TRA, Diana Masalla alisema jana kuwa maeneo ambayo wanawaelimisha wafanyabiashara hao wa China ni ulipaji wa kodi ya mapato, ulipaji wa kodi ya ufundi stadi, ulipaji wa kodi wanayokatwa wafanyakazi (PAYEE) na matumizi ya mashine za malipo za kielektroniki (EFDs).

    Aidha amesema pia, watawaelimisha taratibu za kupata vibali vya kuishi nchini na kufanya kazi nchini, namna ya kulipa kodi kwa biashara wanayofanya na wafuate taratibu zingine za nchi ili wasiingie kwenye matatizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako