• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Benki zinaangalia faini y ash milioni 20 kwa kudanganya wateja wake wanaochukua mikopo

    (GMT+08:00) 2017-07-19 19:07:09
    Benki Kuu ya Kenya (CBK) imechapisha kanuni mpya ambayo itaona benki za kibiashara zikilipa faini ya kushindwa kufichua gharama ya kweli ya mikopo kwa wateja.

    Kanuni mpya ya adhabu kwa benki zote, kampuni za kuuza nyumba na ofisi za mikopo inaonyesha kuwa CBK itaweka adhabu ya juu ya Sh milioni 20 kwa kila ukiukwaji wowote unaotokana na malalamiko ya wateja juu ya mashtaka na kesi nyingine za kutofuatana na Sheria na kanuni za benki.

    Ukiukwaji huu, ni pamoja na kulipa riba, Kushindwa kufichua gharama zote za mkopo au fedha ngapi mteja anapaswa kulipa, ongezeko la malipo yoyote kwa bidhaa au huduma yoyote bila idhini ya maandishi hizo ndio baadhi ya masharti mapya kutoka kwa benki kuu ya Kenya.

    Kanuni mpya zimewekwa ili sheria ya fedha ya 2016 kuanza kufanya kazi.

    Sheria hii ya fedha iliongeza faini kwa ukiukwaji wa sheria kutoka sh milioni Sh5.

    Watu watakao patikana katika uvunjaji wa sheria watalipa faini ya juu ya sh milioni 1 kutoka sh 200,000.

    benki ambazo hazitakubaliana pia zitalipa adhabu ya kila siku ya Sh100,000 kutoka Sh20,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako