Wanawake hao ambao wengi wanavuka mipaka maeneo ya Rusizi-Bukavu na Rubavu-Goma wanalalamikia kuongezeka kwa ufisadi, dhuluma za kingono na ukosefu wa mtaji wa kutosha wa kufanya biashara.
Mwenyekiti wa chama cha wanaouza nyanya na kitunguu Janet Mukamunana amesema matukio hayo yameathiri vibaya biashara zao.
Amesema pia imekuwa vigumu kushindana na wenzao wa DR Congo ambao pia wana bidhaa sawa na zao.
Wengi wa wanawake wanafuka mipaka kufanya biashara ndogondogo kama vile kuuza samaki, maziwa, nyanya na matunda.
Sasa wizara ya biashara viwanda na maswala ya Afrika Mashariki pamoja na wizara ya maswala ya kijinsia zimemesa zinajitahidi kuboresha mazingira ya biashara kwa wanawake hao .
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |