• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Iran asema Iran itajibu vikwazo vya Marekani

  (GMT+08:00) 2017-07-20 10:10:18

  Kufuatia Rais Donald Trump kutangaza vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Iran kutokana na mpango wake wa makombora, Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema Iran itachukua hatua madhubuti kujibu vikwazo vyovyote itakavyowekewa na Marekani kwa kisingizo chochote, na bunge la Iran litapitisha mswada husika kulingana na hatua zitakazochukuliwa na bunge la Marekani.

  Rais Rouhani amesema Iran imetekeleza mkataba kuhusu suala la nyuklia la Iran iliosaini na nchi nyingine sita, lakini Marekani haijatekeleza wajibu wake, ukiwemo kupinga Makubaliano ya Paris na kutoafikiana na Cuba, hali inayoonyesha kwamba Marekani imeshindwa kuwa mhimizaji wa haki za binadamu, utulivu na usalama wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako