• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tetesi ya soka barani Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-07-20 12:02:13

    Chelsea wamefikia makubaliano kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata kwa ada inayoripotiwa kuwa pauni millioni 70.

    Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uhispania sasa anatakiwa kuafikiana masuala yake ya kibinafsi na klabu hiyo na pia achunguzwe hali yake ya kiafya kabla ya kukamilisha uhamisho wake.

    Kwingineko, kipa wa Arsenal kutoka Poland Wojciech Szczesny amehamia katika kalbu ya Juventus ya Italia kwa pauni millioni 10.

    Mlinda lango huyo wa miaka 27 alikaa miaka miwili iliyopita kwa mkopo katika klabu ya Roma. Sasa, ametia saini mkataba wa kudumu wa miaka minne katika mabingwa wa Italia, Juventus.

    Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amethibitisha hana mpango wa kuuza mshambuliaji wake Sergio Aguero kun.

    Guardiola anasema Aguero atabakia City wakati akizungumzia tetesi kuwa huenda mchezaji huyo akaondoka.

    Hatimaye, klabu ya Arsenal inayocheza Ligi Kuu ya England imeandikisha ushindi wa jumla ya 4-3 kupitia mikwaju ya penalti dhidi ya miamba wa Ujerumani Bayern Munich.

    Walipata ushindi huo kwenye mechi ya kirafiki iliyochezewa mjini Shanghai, China.

    Mechi ilikuwa imemalizika 1-1 muda wa kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako