• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiprotich na Kipsiro kukosa mashindano London

    (GMT+08:00) 2017-07-20 12:02:53

    Uganda itatuma kikosi chake kubwa kabisa kushiriki Mbio za mabingwa wa dunia mwezi ujao jijini London. Hata hivyo kikosi hicho cha wanariadha 20 itakuwa bila wanariadha tajika Stephen Kiprotich na Moses Kipsiro.

    Wanariadha hao wawili wenye uzoefu wa mbio za umbali mrefu, ambao pia wanajivunia medali sita za mashinano hayo, walikuwa wamefuzu kushiriki mbio ndefu lakini wamejiondoa kwa sababu binafsi.

    Kipsiro alifichua kuwa mwili wake hauko tayari kwa ajili ya mashindano hayo huku mwenzake kiprotich akisema akili yake pia haipo kwenye mashindano hayo ya Agosti 4 hadi 13.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako