• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyota wa Kenya huenda wakakosa kushiriki mashindano ya Monaco Diamond League

    (GMT+08:00) 2017-07-20 12:03:13

    Wanariadha nyota kadhaa kutoka Kenya huenda wakakosa mashindano ya Monaco Diamond League Ijumaa kwani vyeti vyao vya usafisi bado vimeshikiliwa kwa Ubalozi wa Uingereza kusubiri maombi ya visa.

    Miongoni mwa wanariadha ambao walifuta usafiri siku ya jumanne baada ya kushindwa kupata pasipoti zao ni bingwa wa dunia kurusha mkuki Julius Yego, ambaye pia ni mshindi wa fedha ya Olympiki katika kurusha mkuki, mshindi wa fedha katika mbio za mita 1500 Elijah Manangoi na mshindi wa medali ya shaba katika mbio za mita 800 olympiki Margaret Nyairera.

    Wanariadha hao wanasema hawana budi ila kutoshiriki mashindano hayo iwapo vyeti vyao vya usafiri hayatatolewa kwa muda ufaao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako