• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Duru ya kwanza ya mazungumzo ya uchumi ya pande zote kati ya China na Marekani yafanyika

  (GMT+08:00) 2017-07-20 19:36:35

  Duru ya kwanza ya mazungumzo ya uchumi ya pande zote kati ya China na Marekani yamefanyika mjini Washington, Marekani.

  Naibu waziri mkuu wa China Bw. Wang Yang, waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Terner Mnuchin na waziri wa biashara wa Marekani Bw. Wilbur Ross wameongoza kwa pamoja mazungumzo hayo.

  Kwenye mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimejadiliana kwa kina na kufikia maoni mengi ya pamoja kuhusu biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili, mpango wa siku 100, na mpango wa mwaka mmoja wa ushirikiano wa kiuchumi, utawala wa uchumi duniani, sera za uchumi wa jumla, fedha na kilimo.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Lu Kang kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema mazungumzo hayo ni yenye uvumbuzi, yanayoshughulikia mambo halisi na ya kiujenzi, matokeo ya yaliyopatikana kwenye mazungumzo hayo yataweka msingi imara kwa ushirikiano kati ya China na Marekani katika siku zijazo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako