• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duru ya pili ya mazungumzo ya Brexit yamalizika bila maendeleo

    (GMT+08:00) 2017-07-21 09:35:12

    Duru ya pili ya mazungumzo ya Brexit iliyofanyika kwa siku nne kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya imemalizika jana mjini Brussels, ambapo pande zote mbili hazijafikia makubaliano kuhusu masuala ya malipo ya Uingereza ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya pamoja na usimamizi wa maslahi ya raia wa pande mbili waliopo katika upande mwingine.

    Katika mkutano na waandishi wa habari, mjumbe wa Uingereza Bw David Davies na mjumbe mkuu wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw Michel Barnier wamesema mazungumzo hayo ya kiujenzi yameweka msingi kwa mazungumzo yatakayofuata. Lakini pande hizo mbili zimetoa maoni tofauti kuhusu masuala makuu.

    Kwa upande wa malipo ya Brexit, Davies amesema kuwa pande zote mbili zinatambua umuhimu wa kuthibitisha wajibu wa kila upande kuhusiana na malipo hayo, na kuhusu suala la usimamizi wa maslahi ya raia, Barnier amesema pande hizo mbili zimekuwa na maoni tofauti kuhusu suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako