• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yaitaka dunia kuiokoa Yemen kutoka mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu

    (GMT+08:00) 2017-07-21 10:10:55

    Jumuiya ya Nchi za Kiarabu AL imetahadharisha kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen, ikiitaka jumuiya ya kimataifa kuitikia wito wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wa kudhibiti ugonjwa huo.

    Katibu mkuu wa jumuiya hiyo Bw. Ahmed Aboul-Gheit amezitaka nchi mbalimbali duniani na mashirika ya kijamii kuitikia wito uliotolewa na Shirika la Afya Duniani WHO, Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF ya kukusanya dola milioni 22 za kimarekani ambazo milioni 16 inahitajika kwa dharura ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.

    Bw. Aboul-Gheit amesema, ni lazima kushirikiana kudhibiti ugonjwa huo wa kuambukiza na kuuzuia usienee zaidi nchini Yemen, ili kuepusha mgogoro wa kibinadamu ambao utaweza kudumu kwa miaka mingi ijayo.

    Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Julai 19 na WHO, zaidi ya watu laki 3.6 wanashukiwa kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen na watu 1,817 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako