• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya Iran yapinga Kuwait kuwafukuza wanadiplomasia wake

    (GMT+08:00) 2017-07-21 10:11:17

    Shirika la habari la Iran Fars limesema, wizara ya mambo ya nje ya Iran imemwita balozi mdogo wa Kuwait nchini humo Bw. Falah al-Hajraf kupinga kitendo cha Kuwait kuwafukuza wanadiplomasia 15 wa Iran.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Bahram Qasemi amesema, tuhuma za serikali ya Kuwait dhidi ya Iran hazina msingi wowote.

    Shirika la habari la Kuwait jana liliripoti kuwa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imeitaka Iran ifunge ofisi ya utamaduni na taasisi nyingine za ubalozi wake nchini Kuwait, na kuwafukuza wanadiplomasia kadhaa wa Iran.

    Taarifa ya wizara hiyo pia imesema,uamuzi huo wa Kuwait unatokana na wanadiplomasia wa Iran kutuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako