• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SportPesa All Stars wadhalilishwa Uispania

    (GMT+08:00) 2017-07-21 11:23:08

    TIMU ya Kenya ya SportPesa Premier League All Stars ilifundishwa jinsi ya kutanda soka baada ya kulimwa 4-0 na klabu kutoka Ligi ya Daraja ya Pili ya Uhispania, Cordoba CF katika mechi ya kirafiki Alhamisi usiku.

    Vijana wa Kocha Stanley Okumbi walifungwa mabao na wachezaji Jonathan Mejia, Sergi Guardiola, Alberto Quiles na Alejandro Alfaro.

    All Stars ilianza kuporomoka baada ya kusimama wima kwa robo saa. Lakini walishindwa kuhimili mashambulizi makali ya Cordoba ambayo ilipata bao la kwanza akika ya 20. Mechi ya pili na mwisho ya All Stars nchini Uhispania itakuwa dhidi ya Sevilla Atletico hapo Julai 22.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako