• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli ya Ethiopia na Djibouti kuanzisha huduma mwezi Oktoba

    (GMT+08:00) 2017-07-21 12:26:45

    Wizara ya uchukuzi ya Ethiopia jana imesema reli ya Ethiopia na Djibouti itaanzisha huduma rasmi mwezi Oktoba mwaka huu.

    Waziri wa uchukuzi wa Ethiopia Ahmed Shide amesema, mradi wa reli hiyo ni ishara ya uungaji mkono wa China kwa ajili ya juhudi za Ethiopia katika mageuzi ya uchumi kwa kupitia maendeleo ya miundo mbinu. Amesema, kwa sasa Ethiopia inafanya majaribio ya reli hiyo na kukamilisha maandalizi ya kuunda kampuni ya ubia pamoja na Djibouti ili kuendesha reli hiyo.

    Reli hiyo yenye urefu wa kilomita 756 ilijengwa kwa msaada wa China, na inatarajiwa kupunguza muda wa kusafirisha bidhaa kutoka Ethiopia kwenda bandari ya Djibouti kuwa saa 10 kutoka muda wa siku mbili wa zamani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako