• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaamini nchi za Ghuba zina uwezo wa kutatua migongano ndani ya mfumo wa Kamati ya ushirikiano wa nchi za Ghuba

    (GMT+08:00) 2017-07-21 12:27:14

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana amekutana na mwenzake wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani.

    Bw. Wang Yi amesema, anaamini nchi za Ghuba zina uwezo wa kudhibiti hali ya sasa, na kutatua migongano ndani ya mfumo wa kamati ya ushirikiano wa nchi za Ghuba. Amesema kuwa, pande mbalimbali zinapaswa kujizuia, ili kupunguza hali ya wasiwasi, kufanya mazungumzo haraka iwezekanavyo, kuonyesha ishara ya kushikilia kutatua suala hilo kwa njia ya kisiasa na kidiplomasia, na kurejesha imani kwa kamati ya ushirikiano wa nchi za Ghuba. Bw. Wang Yi pia amesema, China ikiwa ni rafiki wa dhati wa nchi za kiarabu, inapenda kutoa mchango wa kiujenzi katika kuhimiza mazungumzo wakati inapohitajika.

    Kwa upande wake, Al Thani amesema anatumai suala hilo litatatuliwa kwa njia ya mazungumzo. Pia amesema nchi yake inapenda kuanzisha mazungumzo na pande husika, kujenga uaminifu hatua kwa hatua, ili kutatua migongano kimsingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako