• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taarifa kuhusu kifo cha Rais wa zamani wa Zambia zakanushwa

    (GMT+08:00) 2017-07-21 18:41:45

    Ofisi ya Rais wa Zambia imekanusha habari kuwa rais wa zamani wa Zambia Bw Kenneth Kaunda amefariki dunia.

    Baadhi ya habari kwenye mtandao wa internet zilikuwa zinasema Bw Kaunda mwenye umri wa miaka 93 amefariki dunia katika hospitali ya chuo kikuu, alikokuwa amepelekwa kwa matibabu baada ya kulalamika kuwa mgonjwa.

    Msemaji wa ikulu ya Zambia Bw Amos Chanda amekanusha uvumi huo na kusema Bw Kaunda yuko hai lakini yuko hospitali. Amesema Bw Kaunda amepatiwa matibabu na madaktari wamesema anaweza kuondoka, lakini bado yuko hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi.

    Ofisa wa zamani wa serikali ya Kaunda Bw Rodrick Ngolo pia amethibitisha kuwa Bw KK bado ana nguvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako