• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatangaza kusimamisha kwa muda kupokea wakimbizi kutoka Burundi

    (GMT+08:00) 2017-07-21 18:43:11

    Ikulu ya Tanzania imetoa taarifa kuwa baada ya rais John Magufuli wa nchi hiyo kukutana na mwenzake wa Burundi Pierre Nkurunziza, Tanzaina itasimamisha kwa muda kupokea wakimbizi kutoka Burundi.

    Taarifa hiyo imesema, rais Nkurunziza ameshukuru Tanzania kwa kupokea wakimbizi wengi kutoka Burundi na kutoa wito kwa wakimbizi hao kurudia nyumbani na kujenga kwa pamoja taifa lao.

    Habari zinasema Tanzania ni nchi inayopokea wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi. Hivi sasa imeshapokea wakimbizi zaidi ya laki 2.4. Katika miezi mitano ya mwaka 2017, Tanzania imepokea wakimbizi elfu 44 kutoka Burundi, miongoni mwao, asilimia 60 ni watoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako