• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Umoja wa Mataifa aitaka Sudan Kusini irudi kwenye amani

    (GMT+08:00) 2017-07-21 18:43:22

    Msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia ulinzi wa amani Bw El Ghassim Wane amesema changamoto zinazoikabili Sudan Kusini zinatakiwa kuondolewa, ili kutumia fursa ya uwepo wa vikosi vya ulinzi wa usalama kuirudisha nchi hiyo kwenye hali ya utulivu na usalama.

    Bw Wane ameonya kuwa kwa sasa hali ya usalama bado ni dhaifu, na kusema Sudan Kusini inahitaji usimamishaji vita halisi na wenye kuaminika. Ameongeza kuwa kila juhudi inatakiwa kufanywa kuhakikisha kuwa "mjadala wa kitaifa" unakuwa shirikishi, wazi na unafanyika katika mazingira huru na salama, na kuungwa mkono kwa maafikiano makubwa ya kisiasa.

    Pia ameitaka jumuiya ya kimataifa kuifahamisha serikali ya Sudan Kusini kuwa hali ya sasa haikuibaliki na si ya kudumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako