• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burundi yazindua kitivo cha kwanza cha shahada ya udaktari

    (GMT+08:00) 2017-07-21 18:44:25

    Makamu wa pili wa rais wa Burundi Bw. Joseph Butore amezindua kitivo cha kwanza cha shahada ya udaktari nchini humo katika Chuo Kikuu cha Burundi.

    Kwenye hafla ya kuzindua kitivo hiki iliyofanyika katika kampasi ya Kiriri ya Chuo Kikuu cha Burundi, Bw. Butore amesema kitivo hicho kitatoa program kuhusu sayansi jamii, sayansi ya viumbe n.k.

    Amesema kuzinduliwa kwa kitivo hiki ni muhimu kwa chuo kikuu hicho na juhudi za nchi hiyo katika kuendeleza utafiti wa kisayansi.

    Chuo Kikuu cha Burundi ni chuo pekee cha umma nchi humo kinachogharamiwa na serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako