• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni 115 ya China yaingiakwenye orodha ya makampuni 500 yenye nguvu na gazeti la Fortune

    (GMT+08:00) 2017-07-21 18:46:12

    Gazeti la Fortune la Marekani limetoa orodha ya makampuni 500 yenye nguvu kubwa zaidi kwa mwaka 2017.

    Makampuni 115 ya China yamo kwenye orodha hiyo, idadi ambayo imeongezeka kwa makampuni matano kuliko ile ya mwaka jana, na kuchukua nafasi ya pili duniani baada ya Marekani.

    Hii ni mara ya kwanza kwa makampuni 10 yakiwemo kampuni ya hisa ya Anbang, kampuni ya Alibaba na kampuni ya Tencent kuingia kwenye orodha hii.

    Makampuni 132 ya Marekani yameingia kwenye orodha hiyo, na kampuni ya Walmart inachukua nafasi ya kwanza kwa mapato ya dola za kimarekani bilioni 485.873, nafasi za pili hadi nne zinachukuliwa na makampuni ya China yakiwemo Shirika la umeme la China, na mashirika ya mafuta Sinopec na CNPC, na ya tano inachukuliwa na kampuni ya magari ya Toyota ya Japan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako