• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanya biashara kutoka Uganda wapongeza mabadiliko kwenye bandari ya Mombasa

    (GMT+08:00) 2017-07-21 19:33:57

    Wafanyabiashara kutoka Uganda wamepongeza mamlaka ya bandari ya Kenya kwa kuondoa vikwazo vya kuondoa mzigo walivyokuwa wakishuhudia hapo awali. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara hao Bw Ezra Rubanda, wafanya biashara wa Uganda wameona mabadiliko makubwa sana kwenye biashara zao kutokana na urahisi wa kuondoa mzigo bandarini humo. Bwana Rubanda ameongeza kuwa awali ilikuwa vigumu kufanya biashara kutokana na changamoto nyingi tu ikiwemo kupotea kwa mizigo. Rubanda pia ameongeza kuwa muda wa kusafirisha mizigo umeboreshwa kutoka siku 24 hadi siku 5 hivi sasa.Mwaka jana, bandari ya mombasa ilishughulikia jumla ya tani milioni 27.36 ya mizigo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako