• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya ngano yapanda nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2017-07-21 19:34:18

    Wizara ya kilimo ya Kenya imetangaza bei mpya ya ngano kutoka shilingi elfu 3 hadi shilingi elfu 3400 kwa gunia la kilo 90.Tangazo hilo linakuja wakati ambapo uzalishaji wa ngano unatarajiwa kushuka kwa asilimia 50 kutokana na ukosefu wa mvua.Akizungumza na waandishi wa habari, katibu wa kudumu wa Wizara ya kilimo wa Kenya Bw Richard Lesiyampe amesema upungufu wa mvuo umepelekea uzalishaji wa zao hilo kupungua kwa nusu hadi ikilinganishwa na mwaka jana ambapo wakulima walifanikiwa kuzalisha magunia milioni 3. Msimu wa kwanza wa mavuno unaendelea hivi sasa kusini mwa Kenya ambapo uzalishaji wa zao hilo unatarajiwa kushuka hadi milioni 1.2. Bw Lesiyampe ameongeza kuwa serikali itaagiza zaidi ya asilimia 70 ya nafaka ili kuziba pengo lililopo hivi sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako