• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Facebook kudhibiti taarifa zinazochapishwa bila malipo

    (GMT+08:00) 2017-07-21 19:37:11

    Kampuni ya Facebook imesema itafanya uchunguzi kuhusiana na suala la kudhibiti idadi ya taarifa za habari zinazochapishwa na kusomwa bila malipo kwenye mtandao huo. Taarifa hii inakuja wakati ambapo Facebook imekuwa chanzo muhimu cha habari kwa watu wengi hali ambayo imezua malalamishi kutoka kwa wachapishaji wanaodai kupoteza fedha nyingi na udhibiti wakati habari zao zinaenezwa bure katika mtandao wa Facebook. Kutokana na taarifa hiyo, wanaoweka taarifa watakuwa wakilipia kutokana na kuwa kampuni hiyo inazindua mfumo wa kulipa kwanza kabla ya kuweka taarifa. Huduma hiyo ilianzishwa miaka miwili iliyopita na inashindana na huduma ya Google ya AMP ambayo hutumia habari kutoka kwa mashirika yaliyochaguliwa na ambayo habari zake zinaweza kupatikana kwa njia ya simu. Akizungumza na wanahabari, msimamizi wa kitengo cha ushirika wa habari cha Fecebook Campbell Brown amesema kampuni hiyo inachukulia kwa umuhimu mkubwa malalmishi ya wachapishaji. Kuanzia Octoba mwaka huu, Facebook itaanza kukagua mfumo huo unaodhibiti hadi jumla ya habari kumi zinazoweza kupatikana bila malipo kupitia mtandao wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako