• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani azitaka nchi nne kuondoa vizuizi dhidi ya Qatar

    (GMT+08:00) 2017-07-22 16:07:37

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson amesema Qatar imeonesha msimamo mzuri kwenye mapambano dhidi ya ugaidi, na Marekani inatarajia nchi nne za Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri kuondoa vizuizi dhidi ya Qatar mapema iwezavyo.

    Bw. Rex Tillerson na mwenzake wa Amman Bw. Youssef Alawi Bin Abdullah ambaye yuko ziarani nchini Marekani walipokutana kwa pamoja na waandishi wa habari, Bw. Tillerson amesema Qatar imetekeleza kwa makini kumbukumbu za maelewano zilizosainiwa na nchi hiyo na Marekani kuhusu kupambana na vitendo vya kufadhili ugaidi, pia imeonesha nia ya kufanya majadiliano na nchi nne zilizoiwekea vizuizi, hivyo Marekani inatarajia nchi hizo zitaondoa vizuizi hivyo ambavyo zimeathiri vibaya maisha ya wananchi wa Qatar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako