• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijana sita wa Burundi wamepotea baada ya kuhudhuria mashindano ya robot nchini Marekani.

    (GMT+08:00) 2017-07-22 16:12:37

    Vijana sita kutoka Burundi wamepotea baada ya kuhudhuria mashindano ya robot ya kimataifa yaliyofanyika mjini Washington Marekani mapema wiki hii, na wawili wao wameripotiwa kuingia Canada.

    Kwa mujibu wa taarifa toka mamlaka ya Canada inasema, wavulana wanne na wasichana wawili ambao walishiriki katika mashindano hayo walionekana Jumanne jioni baada ya msimu wa kwanza wa kimataifa kumalizika.

    Polisi imetoa picha za waliopotea, huku msemaji wa polisi mjini Washington D.C amewataja kijana Audrey Mwamikazi mwenye umri wa miaka 17 na Don Ingaribe mwenye umri wa miaka 16 walionekana kuvuka mpaka wa Marekani kwenda Canada bila kutoa maelezo juu ya jinsi Waburundi wawili walivyoona au sababu ya kuvuka kwa mpaka.

    Nao waandaaji wa mashindano hayo wamesema vijana hao, walipewa viza ya mwaka mmoja, na waliweka funguo za vyumba kwenye mfuko wa msimamizi na kuondoka na nguo zao.

    Mamlaka ya Canada imesema hawawezi kuthibitisha wala kukataa juu ya vijana hao kuripotiwa kuingia nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako