• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Mahmoud Abbas wa Palestina atangaza kukatisha mawasiliano kati ya Palestina na Israel mara moja

    (GMT+08:00) 2017-07-22 17:19:01

    Rais Mahmoud Abbas wa Palestina jana usiku ametangaza kuwa Palestina itakatisha mawasiliano na serikali ya Israel mara moja katika sekta zote mpaka Israel itakaposimamisha vitendo dhidi ya eneo la kuheshimiwa la kiislam kwenye mji mkongwe wa Jerusalem.

    Rais Abbas usiku huo aliitisha mkutano wa dharura ikulu ya Palestina, maaofisa wa ngazi ya juu wa kundi la ukombozi la Palestina, kundi la Fatah la Palestina, idara ya usalama ya Palestina walihudhuria mkutano huo. Baada ya mkutano huo, rais Abbas alisema kuwa, Palestina inaipinga Israel iweke vifaa vya kung'amua vyuma kwenye mlango wa eneo takatifu la Haram al Sharif. Kitendo cha Israel kiliharibu mchakato wa amani, na kuhimiza mgogoro wa siasa kati ya Palestina na Israel kuwa mgogoro wa dini.

    Siku hiyo, jeshi la ulinzi wa taifa la Israel lilisema kuwa, tukio la kuwashambulia waisrael kwa mpalestina kwenye makazi ya wayahudi magharibi mwa mto Jordan na kusababisha vifo vya waisrael watatu na mwengine mmoja kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako