• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama nchini Misri yathibitisha hukumu ya vifo kwa watu 28 waliohusika na mauaji ya mwendesha mashtaka mkuu wa zamani

    (GMT+08:00) 2017-07-22 18:56:38

    Mahakama nchini Misri jana imethibitisha hukumu ya kifo kwa watu 28 waliohusika na mauaji ya mwendesha mashtaka mkuu wa zamani mwaka 2015.

    Kwa mujibu wa televisheni ya taifa ya nchi hiyo imesema, mahakama ya jinai mjini Cairo pia imewahukumu watu 15 kifungo cha maisha ambayo ni sawa na miaka 25 huko Misri, watu wanane kifungo cha miaka 15, na wengine 15 kifungo cha miaka 10 kwa kesi hiyo.

    Washitakiwa hao walikutwa na hatia ya majaribio ya mauaji, kushirikiana na kikundi cha kigaidi na kumiliki silaha na mabomu.

    Mwendesha mashtaka wa zamani Hisham Barakat aliuawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari mjini Cairo Juni 29, mwaka 2015. Kikundi kinachojulikana na watu wachache kikijiita "Upinzani maarufu wa Giza" kilidai kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako