Mwongozaji mkuu wa upande wa China ambaye pia ni naibu kamanda wa jeshi la baharini Bw. Tian Zhong akitoa risala kwenye ufunguzi huo amesema, luteka hiyo ni hatua halisi ya kuimarisha uhusiano wa ushirikiano na wa kiwenzi kwa pande zote, ambayo inasaidia kulinda kwa pamoja amani ya dunia na utulivu kwenye kanda hiyo. Ameongeza kuwa, luteka hiyo kwa mwaka huu itaweka mkazo katika kukabiliana na matishio ya kigaidi na utoaji wa misaada ya dharura zinazokumba mambo ya kiuchumi baharini ya nchi mbalimbali, kuinua ngazi ya mawasiliano kati ya pande hizo mbili ili kuhimiza kiwango cha ushirikiano na uwezo wa kufanya operesheni kwa pamoja kati ya majeshi ya nchi hizo mbili.
Mwongozaji mkuu wa luteka hiyo wa upande wa Russia Bw. Aleksandr Dedotenkov amesema, luteka hiyo ya mwaka huu itahimiza ushirikiano na uhusiano wa kirafiki kati ya majeshi ya nchi hizo mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |