• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Marekani lapanga kupitisha muswada kuhusu kuziwekea vikwazo Russia, Iran na Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-07-23 18:16:36
    Bunge la Marekani limetangaza kuwa, baraza la chini na la juu la bunge hilo yatahimiza kwa pamoja kupitishwa kwa muswada kuhusu kuziwekea vikwazo Russia, Iran na Korea Kaskazini, endapo pendekezo hilo litapitishwa, litawasilishwa kwa rais Donald Trump mwishoni mwa mwezi huu.

    Mbali na mambo kuhusu uwekaji wa vikwazo, muswada huo vilevile unaweka mipaka kwa madaraka ya rais kuhusu kuondolea vikwazo Russia. Kwa mujibu wa muswada huo, rais atakapotoa uamuzi kuhusu sera za kidiplomasia zinazohusu Russia anatakiwa kutoa ripoti kwa bunge, wakati bunge lina haki ya kukataza uamuzi wa rais.

    Kutokana na mpango uliowekwa, baraza la chini la bunge litapiga kura kuhusu muswada huo tarehe 25, ikiwa utapitishwa litawasilishwa kwenye baraza la juu la bunge, na baada ya hapo kuwasilishwa kwa rais Trump na kuamuliwa nae kama utapitishwa na kuwa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako