Afrika Kusini bado inashikilia uamuzi wa kujitoa katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC).
Mwenyekiti wa kamati ndogo ya uhusiano wa kimataifa wa chama cha tawala cha African Congress (ANC) Bi Edna Molewa ambaye pia ni waziri wa maji na uhusiano wa mazingira ameeleza kuwa mahakama hiyo ilihimiza Afrika Kusini kuchagua kati ya kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Roma na kukamata mkuu wa serikali hiyo wakati akihudhuria mkutano kama mgeni wa Umoja wa Afrika. Uamuzi ambao amesema kuwa na madhara makubwa na uwezekano wa hatari ya sera za kigeni.
Mahakama ya kimataifa iliitaka Afrika Kusini kumkamata Rais wa Sudani Al-Bashir alipoingia nchini humo mwezi Juni mwaka 2015 kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |