Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC jana ilitoa taarifa ikieleza wasiwasi kutokana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen. Taarifa ya kamati hiyo imetahadharisha kuwa kama hatua madhubuti hazitachukuliwa, maambukizi ya kipindupindu nchini humo yatafikia laki sita ifikapo mwishoni mwa mwaka, yaani moja kati ya watu 45 nchini humo ataambukizwa ugonjwa huo. Takwimu zilizotolewa na ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA zinaonesha kuwa maambukizi ya kipindupindu yameathiri kila jimbo nchini Yemen na kusababisha vifo vya watu 1,780.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |