• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watafiti wa kisayansi wa Afrika Mashariki na wa Umoja wa Ulaya kukabiliana na athari za fluoride kwa afya ya binadamu

    (GMT+08:00) 2017-07-24 09:45:16

    Watafiti wa kisayansi kutoka Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya (EU) wameanza kufanya utafiti yakinifu kuhusu njia za kukabiliana na athari za afya zinazosababishwa na flouride kwa afya ya binadamu kupitia maji.

    Mhandisi wa maji Mkoa wa Arusha Bw Joseph Makaidi, amesema Tanzania bado haijapata teknolojia yenye ufanisi ili kuondoa flouride kutoka kwenye maji kwa ajili ya matumizi ya ndani.

    Naye Bwana Giogio Ghighler mtafiti kiongozi kutoka chuo kikuu cha Cagliari cha Italia, amesema fluoride pia imeathiri wanyama, lakini ameongeza kuwa, hakuna matokeo ya utafiti kamili yaliyofanyika juu ya athari zake kwa binadamu.

    Flouride iliyopo kwenye maji kwa miaka mingi imeathiri afya ya wakazi wa Arumeru mkoa wa Arusha kudhoofisha mifupa yao, ikiwa ni pamoja na meno na wakati mwingine husababisha ulemavu wa mwili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako