• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya aahidi mamilioni ya ajira katika kipindi cha miaka mitano

    (GMT+08:00) 2017-07-24 09:45:44

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anayegombea kuchaguliwa kuwa rais wa Kenya kwa muhula mwingine, ameahidi kuwa serikali yake itaongeza nafasi milioni 6.5 za ajira hasa kwa vijana, na kupunguza bei za vitu katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

    Rais Kenyatta aliyekuwa anajibu maswali moja kwa moja kupitia facebook kuhusu mipango ya serikali yake kama akichaguliwa, amesema mpango wake utaleta mabadiliko kwenye mafanikio yaliyopatikana katika miaka minne iliyopita.

    Mbali na nafasi za ajira, Rais Kenyatta pia amesema atapambana na ufisadi, na kuhakikisha kuwa mahakama inatekeleza wajibu wake ili wahalifu wachukuliwe hatua.

    Rais Kenyatta pia ametaka usalama uimarishwe kabla, wakati na baada ya uchaguzi, na kuwakumbusha wakenya kufuata kanuni ya umoja, demokrasia na kuishi kwa masikilizano wakati wakijiandaa na uchaguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako