• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yaonya mashirika ya utumaji pesa kuhusu kuwafadhili magaidi

    (GMT+08:00) 2017-07-24 09:46:06

    Somalia imeonya makampuni ya utumaji wa fedha kutosaidia kutuma fedha zinazofadhili shughuli za kigaidi nchini humo.

    Waziri wa usalama wa ndani wa Somalia Bw Mohamed Abukar Islow amesema, serikali imepitisha amri ya kuzuia benki na makampuni yanayotumia fedha za kulisaidia kundi la Al Shabaab, na kuonya watakaokiuka sheria hiyo.

    Uamuzi wa serikali umepitishwa kufuatia habari kuwa kundi la Al shabaab linawatoza faini wafanyabiashara na kutuma fedha kupitia makampuni ya utumaji wa fedha. Serikali pia imewaonya watu wanaolipa faini kwa kundi la Al Shabaab.

    Mkuu wa idara ya usalama ya Somalia NISA Bw Abdulahi Ali amesema serikali utafuatilia utumaji pesa unaofanywa na makampuni nchini Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako