• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Syria na Chama cha Hezbollah cha Lebanon wapambana na Kundi la Nusra Front

    (GMT+08:00) 2017-07-24 09:58:58

    Jeshi la Syria na Chama cha Hezbollah cha Lebanon wamepambana na Kundi la Nusra Front lenye uhusiano na Kundi la Al-Qaida katika eneo la Qalamoun karibu na mpaka kati ya Lebanon na Syria.

    Shirika la uangalizi wa haki za binadamu nchini Syria limesema baada ya vikosi vya Syria na Chama cha Hezbollah kuanzisha msako huko Fleita, mapambano yametokea katika eneo la Qalamoun, kaskazini magharibi mwa Damascus karibu na mpaka wa Lebanon.

    Shirika hilo pia limesema baada ya kumaliza msako dhidi ya waasi hao, jeshi la Syria litatwaa tena udhibiti wa maeneo yote magharibi mwa Qalamoun.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako