• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika kuanzisha kampeni ya upatikanaji maji safi na usafi katika nchi nne

    (GMT+08:00) 2017-07-24 10:06:45

    Mfuko wa hisani ya afya wa Afrika, shirika la AMREF Afrika na Mfuko wa Coca Cola wa Afrika, wametangaza mradi wa pamoja wa kuhimiza upatikanaji wa maji safi na usafi nchini Kenya, Uganda, Tanzania na Ethiopia.

    Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Jumamosi usiku, Mfuko wa Coca Cola wa Afrika utatoa dola milioni 4.2 za kimarekani kusaidia mfuko wa afya wa Afrika wa AMREF wenye makao yake Nairobi kutekeleza miradi inayoharakisha upatikanaji wa maji safi ya kunywa na usafi wa mazingira kwa takriban watu laki 5 katika nchi hizo nne.

    Akipongeza ushirikiano huo katibu mkuu wa wizara ya maji ya Kenya Bw Fred Segor amesema mradi utaleta matokeo chanya katika afya na uchumi kwenye jamii za kanda hiyo. Aidha amesema jamii zisizonufaika kwenye mikoa kame na mitaa ya mabanda ya Kenya nazo pia zitanufaika na mpango huo wa kupanua upatikanaji wa maji safi na usafi.

    Naye rais wa mfuko wa Coca Cola wa Afrika, Bi Susan Mboya amesema mpango huo unalenga kufikia watu milioni sita barani Afrika..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako