Umoja wa nchi za Kiarabu utaitisha mkutano wa dharura wa ngazi ya mawaziri tarehe 26 mwezi huu, kujadili hali ya uhusiano kati ya Israel na Palestina.
Katibu mkuu wa umoja huo Bw Ahmed Aboul Gheit amesema, hatua zilizochukuliwa na serikali ya Israel haziendani na mahitaji ya usalama, bali ni kitendo cha uchokozi kinachoweza kusababisha mgogoro mkubwa kati yake na waislam. Amesisitiza kuwa nchi za kiarabu na waislam hawawezi kukubali kitendo chake katika mji wa Jerusalem.
Habari zinasema Israel ilipiga marufuku waislam kuingia kwenye eneo la Temple Mount kufanya ibada kutokana na vifo vya polisi wawili katika eneo hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |