• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uturuki awasili Saudi Arabia kusuluhisha mgogoro wa kidiplomasia wa Qatar

    (GMT+08:00) 2017-07-24 10:19:29

    Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amewasili Jeddah, Saudi Arabia kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro wa kidiplomasia kati ya Qatari na nchi nne.

    Kwenye ziara hiyo, Rais Erdogan amezungumza na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz Al Saud. Baadaye atafanya mazungumzo na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Mohammad bin Salman .

    Rais Erdogan amesema, kupamba moto kwa mgogoro huo hakunufaishi upande wowote. Amesema Uturuki inaunga mkono suala hilo litatuliwe mara moja. Pia amesifu msimamo wa Qatar wa kujizuia kwenye mgogoro huo, na kusema imetoa mchango wa dhati kwa ajili ya utatuzi wa suala hilo kwa njia ya mazungumzo.

    Habari zinasema, baada ya ziara nchini Saudi Arabia, rais Erdogan pia atatembelea Kuwait na Qatar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako