• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya Kiplagat, Chepkirui washinda dhahabu Bahamas

    (GMT+08:00) 2017-07-24 10:39:00
    Wakenya Edwin Kiplagat na Emmaculate Chepkirui Jumamosi walifagilia ushindi katika mashindano ya chipukizi ya Commonwealth ya wavulana na wasichana ya mita 3,000 yaliyokamilika Jumapili nchini Bahamas.

    Chepkirui, ambaye ametoka kujishindia medali ya fedha katika mbio za mita 3,000 katika mashindano ya chipukizi wasiozidi miaka 18 wiki iliyopita jijini Nairobi, aliongoza na kumiliki mbio hizo kwa dakika 9 na sekunde 25.40.

    Chepkirui, alimpiku Katrina Robinson kutoka New Zealand aliyechukua nafasi ya pili naye Brogan MacDougall kutoka Canada akamaliza msururu wa tatu bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako