• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Amavubi Stars kuchuana na Uganda Cranes

    (GMT+08:00) 2017-07-24 10:39:21
    Baada ya kubandua timu ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars katika raundi ya pili ya kufuzu kwa mashindano ya CHAN, Amavubi stars ya Rwanda sasa imejikatia tikiti ya kuchuana na vijana wa Cranes kutoka Uganda.

    Rwanda iliiondoa Tanzania kwa jumla ya bao 1-1 baada ya kutoka sare katika mechi ya marudiano kwenye uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali. Hivyo basi, Rwanda imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini, walilolipata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Mwanza

    Uganda ilifuzu kuingia awamu hiyo ya tatu na ya mwisho baada ya kuitinga timu ya soka ya Sudan Kusini bao 5-1 siku ya Jumamosi mjini Juba. Mshindi wa mechi hii atafuzu moja kwa moja kwa fainali za CHAN ambazo zimepangwa kupigwa nchini Kenya mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako