• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha Micho Sredojevic kugura Cranes

    (GMT+08:00) 2017-07-24 10:39:44
    Mkufunzi wa timu ya soka ya taifa ya Uganda Micho Sredojevic ametangaza nia yake ya kutoendelea kuifunza timu ya Cranes kutokana na kutokuelewana baina yake na usimamizi wa soka nchini humo.

    Micho alinakiliwa baada ya kuiongoza timu yake kushinda Sudan Kusini akidai kuwa matakwa yake hayajashughulikiwa ipasavyo na shirikisho la soka nchini Uganda FUFA.

    Inasemekana kuwa chanzo cha ugomvi baina ya raia huyo wa Serbia na shirikisho hilo ni mtafaruku unaozingira malimbikizo yake hata ingawa FUFA inashikilia msimamo wake kuwa haina deni la kocha huyo.

    Aidha, rais wa FUFA Moses Magogo, amefutilia mbali tetesi kuwa kocha huyo amewasilisha barua ya kutaka kugura wajibu wake kama kocha wa Cranes.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako