• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Froome ashinda kombe ya Tour de France kwa mara ya nne

    (GMT+08:00) 2017-07-24 10:40:03
    Muingereza Chris Froome alijinyakulia kombe lake la nne la Tour de France katika hatua ya 21 na ya mwisho iliyoshindwa na Dylan Groenewegen jijini Paris siku ya Jumapili.

    Froome, anayewakilisha Sky, hapo awali alishinda matoleo ya mwaka 2013, 2015 na 2016 na sasa anashikilia nafasi ya tano kwa orodha jumla ya washindi wa mashindano hayo nyuma ya vigogo Eddy Merckx, Jacques Anquetil, Bernard Hinault na Miguel Indurain.

    Kwa mara ya kwanza Froome alionekana kungangana sana katika mashindano hayo kwani kiasi cha ushindi wake ilikuwa chini ya dakika moja mbele ya raia wa Colombia Rigoberto Uran aliyemaliza wa pili kwa sekunde 54 baadaye. Romain Bardet wa Ufaranza alimaliza wa tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako